Habari

Mbunge viti maalum amlaani Polepole bungeni, adai ni aibu kwa CCM kuwa na kiongozi anayedhalilisha wanawake

Mbunge wa viti Maalumu, Upendo Peneza (CHADEMA) amemtuhumu Katibu Mwenezi kwa CCM, Humphrey Polepole kuwa anadhalilisha wanawake kwa kauli zake kuhusu wabunge wa viti maalumu.

Mhe. Upendo Peneza

Mhe. Peneza amesema kuwa Mwenezi Humphery Polepole, amewadhalilisha wabunge wa viti maalumu wanaotokana na chama chake kuwa wamepata nafasi hizo baada ya kulala na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2019/20, Peneza amesema kuwa wabunge wa viti maalumu wapo kwa mujibu wa Katiba na nashangazwa na kauli zinazotolewa na Polepole za kudai kuwa ‘Wabunge wa viti maalumu CHADEMA hawapiti mpaka wapitiwe na Mwenyekiti wao’ .

Kitu kibaya kinachoendelea ndani ya nchi hii, kilianza ndani ya Bunge hili lakini Mwenyekiti na viongozi wengine walikemea tabia hii ya “kipuuzi”, lakini sasa imefika huko nje ambapo ndugu, Humphrey Polepole amesema wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wanapatikana mpaka “wapitiwe” na Mwenyekiti wao, huu ni udhalilishaji,” amesema Upendo Peneza.

Sasa kama hata hatambui haki za kikatiba ni aibu kwa Chama cha Mapinduzi kuwa na mwenezi anayedhalilisha wanawake,”amesema Peneza na kuendelea “Ifike mahali nafasi walizonazo na vyeo walivyo navyo viheshimiwe. Ni aibu kwa kiongozi wa nchi hii kusimama na kusema kwamba mafanikio ya mwanamke ya kisiasa yanatokana na shughuli za kingono, tunawajengea watoto wetu fikra mbaya ndani ya Vichwa vyao“.

Hata hivyo, bado haijawekwa wazi ni wapi Polepole alitoa kauli hiyo iliyotafsiriwa kama ya udhalilishaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents