Habari

Mbwa wa Biden awauma walinzi wa rais

Mbwa wa rais Joe Biden kwa jina kamanda aliwauma maajenti wa Huduma ya Siri wa Marekani angalau mara 24, hati mpya zinaonyesha.

Rekodi za Huduma ya Siri ya Marekani zinaonyesha ni kwa kiwango ganimbwa huyo aina ya german Shephard alizua vurugu miongoni mwa walinzi wa rais.

Wakala mmoja mkuu alibaini kuumwa kunamaanisha Huduma ya Siri ilibadilisha mbinu, na kuwashauri mawakala “kutoa uhuru mwingi”.

Onyo hilo linajiri miezi kadhaa kabla ya Kamanda huyo kuondolewa Ikulu.

Hati hizo zilifichuliwa kupitia maombi ya Uhuru wa Habari na kuwekwa mtandaoni. Zimeundwa upya ili kulinda utambulisho wa mawakala wa Ujasusi na mbinu zao za usalama.

Wanaonyesha angalau matukio 24 ya kuumwa yalitokea kati ya Oktoba 2022 na Julai 2023, ikiwa ni pamoja na wanachama wa Secret Service kuumwa kwenye kifundo cha mkono, paji la uso, kiwiko, kiuno, kifua, paja na bega.

Hati hizo sio lazima zirekodi matukio yote ya kung’atwa yanayohusiana na Kamanda, kwani yanahusu Huduma ya Siri pekee na sio zingine zinazofanya kazi Ikulu au wafanyikazi wa Camp David huko Maryland.

Mnyama huyo ambaye ni kipenzi cha familia ya Biden aliondoka Ikulu Oktoba mwaka jana, wiki moja baada ya ajenti wa Ujasusi kuhitaji matibabu bada ya kuumwa vibaya.

Tukio la awali mnamo Juni lilisababisha “kuumwa vibaya” kwenye mkono wa wakala, ambaye alihitaji kushonwa. Damu kwenye sakafu katika eneo la Ikulu ilisababisha ziara za Mrengo wa Mashariki wa jengo hilo kusimamishwa kwa dakika 20, kulingana na hati moja.

Mnamo Julai, wakala mwingine aliumwa mkononi na kuhitaji kushonwa nyuzi sita. Kidonda hicho kilisababisha “jeraha kubwa la wazi” na wakala “alianza kupoteza kiasi kikubwa cha damu”, barua pepe moja ilionyesha.

Wakala huyu alipewa “kifurushi cha huduma ndogo” na wenzake kama zawadi ikiwa ni pamoja na dawa za kutuliza maumivu, mafuta ya antibiotiki, dawa ya pilipili, mdomo na biskuti za mbwa “kwa madhumuni ya usalama”.

Ajenti mkuu ambaye hakutajwa jina katika barua pepe moja alishauri kwamba maajenti wanaomlinda Bw Biden na familia yake “lazima wawe wabunifu ili kuhakikisha usalama wetu binafsi”.

“Kung’atwa na mbwa hivi majuzi kumetupa changamoto ya kurekebisha mbinu zetu za kufanya kazi wakati Kamanda yupo – tafadhali kaamba mbali ikiwezekana,” wakala aliandika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents