FahamuHabariMichezo

Mchezaji wa Chelsea ashambuliwa kwa ubaguzi wa rangi kwa mtoto (video)

Moja ya clip inayosambaa kwa haraka mitandaoni ni hii ikimuonuesha Kiungo Mshambuliaji na kapteni wa muda wa Chelsea raia wa Uingereza @conorgallagher92 akionyesha ishara za ubaguzi wa rangi kwa mtoto mwenye rangi nyeusi.

Watu wengi wamemshambulia mchezaji huo baada ya kuukataa mkono wa mtoto huyo ambaye ameonyesha mkono kwa muda mrefu bila mafanikio.

Gallagher alikuwa capteni wa Chelsea dhidi ya klabu ya Burnley na akiwa kama kapteni wakati anatoka amekuta watoto wamejipanga kwa ajili ya kuingia nao uwanjani.

Baada ya kuanza kuwasalimia watoto wale alianza nyuma kabisa na mtoto wa mwisho alikuwa ana rangi nyeusi.

Baada ya kufika kwake Gallagher hakumpa mtoto yule mkono badala yake alimshika shingoni tu lakini mtoto yule hakushusha mkono wake akiamini kuwa Gallagher labda hakuuona mkono wake.

Cha kushangaza alirudisha macho tena kwa mtoto yule hakumpa mkono ila akaendelea kumuangalia na kumsemesha mtoto aliyopo nyuma yake ambaye ni Mzungu.

Katika mchezo huo Chelsea walipata sare ya kufungana goli 2-2 na Burnley licha ya kuwa Burnley walikuwa pungufu baada ya mchezaji wao Assignon kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 40 tu ya mchezo huku chelsea wakiwa mbele kwa goli 1 lililofungwa kwa penati na Palmer.

Unahisi Conor Gallagher hakuuona mkono wa mtoto huyo mweusi au amefanya makusudi??

Written by @el_mando

link ya video https://www.instagram.com/reel/C5NnA13N12F/?igsh=MTc4Mm84OTE4cm5tOQ==

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents