Mchongo wa kusaidia biashara ya Ubunifu Africa

Afrika Mashariki – June 2021 – Mfuko wa kusaidia biashara ya ubunifu Afrika Mashariki wa Heva (EACBF) ni utaratibu wa utoaji mkopo uliowekwa wazi kuanzia 2021 na kuendelea kwa waombaji waliofanikiwa, kupitia uwekezaji wa madeni wa kati ya dola za Kimarekani 20,000 na dola 50,000, kwa kipindi cha zaidi ya miaka 4.

Mfuko huo ambao ni muitikio wa wakati kwa upotevu wa mali na fursa kwa wabunifu wakati wa janga la COVID-19, umetangaza kupokea maombi ya waombaji 76 wenye sifa 76 katika jumla ya maombi 430 kutoka Kenya (248), Uganda (59), Ethiopia (33), Tanzania (30) na Rwanda (60).

Maombi yote yaliyotajwa hapo juu yaliwasilishwa kati ya Septemba na Oktoba 2020, pindi maombi ya EACBF yalipofunguliwa rasmi.

76 kati ya waombaji wote 430 wana sifa za kupewa fedha, wakiwa wamefikia mahitaji yote: Biashara yenye kipato kisichozidi dola 20,000, na mwajiriwa/mfanyakazi takriban mmoja (kama kazi ya ziada ama kazi ya muda wote).

Waombaji wote wenye sifa wamesajiliwa na wanafanya kazi kwenye nchi za Afrika Mashariki kama ifuatavyo: Kenya (40), Uganda (11), Ethiopia (4), Tanzania (7) na Rwanda (14).

Katika makampuni hayo, 28 ni makampuni yanayoendeshwa na wanawake, wakati 43 yanamilikiwa au kuendeshwa na wanaume. Waombaji 5 hawakupenda kuelezea jinsia zao.

Related Articles

Back to top button