HabariSiasa

Mchuano mkali Odinga, Ruto uchaguzi mkuu Kenya

Wakenya wameendelea kusubiri kwa hamu matokeo ya kura ya urais baada ya uchaguzi wa Jumanne kumalizika kwa amani. Matokeo ya awali yanaonesha mchuano mkali baina ya naibu wa rais William Ruto na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga.

Maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC, wameendelea na zoezi la kuhesabu kura huku tume hiyo ikikabiliwa na shinikizo la kutangaza matokeo kufikia Agosti 16.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewatolea wito Wakenya kuwa watulivu, kuepuka madai ya udanganyifu wa kura ambayo yaligubika chaguzi zilizopita.

Wakati matokeo yakiendelea kutolewa, shirika la kimataifa la Amnesty international pamoja na mashirika mengine ya kiraia, yameelezea wasiwasi juu ya kuongezeka kwa habari za uongo na kupotosha haswa katika mitandao ya kijamii.

Kenya ilipiga kura siku ya Jumanne, kumchagua rais, wabunge, maseneta, magavana na wawakilishi wa wanawake.

Source DW.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents