Burudani

Mdundo watoa orodha maalum ya muziki wa kaswida kwaajili ya Mwezi wa Ramadan

Imani na muziki zitaungana pamoja kwenye Mdundo.com ili kukonga nafsi za waumini wote katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan – baada ya huduma hiyo maarufu ya kutiririsha mziki mtandaoni kuzindua ushirikiano wa kipekee na kampuni ya teknologia ya Vodacom pamoja na kituo cha redio Clouds FM.

Mdundo yaitakia waTanzania Ramadhan Kareen na kuwakaribisha katika mwezi mtukufu kwa kuwapatia orodha maalum ya muziki wa Kaswida.

Kwa mara ya kwanza kabisa kuanzia Aprili 1 – 30 msimu huu wa Ramadhan, Kila siku, Mdundo.com inatoa fursa ya kipekee kwa waumini wa dini ya Kiislamu kusikiliza na kupakua mpangilio wa muziki maalum wa Kaswida kutoka kwa maDJ mbalimbali kukuza safari yao ya kiroho.

Maudhui husika yanajumuisha aina mbali za muziki ikiwemo Kaswida, Taarab, Singeli, Injili, Bongo, Naija/Afrobeat, Amapiano, Hip hop na nyingine nyingi.

Clouds FM pia wameungana na Mdundo.com kuwapa wasikilizaji muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maarufu wa Clouds FM, ambao sasa unapatikana kupitia ukurasa wa mdundo.com/cloudsfm- https://mdundo.com/a/258048.

Kwa taarifa zaidi: Follow: IG @mdundomusictz | Twitter: @mdundomusic

“Kwa mara ya kwanza kabisa kuanzia Aprili 1 – 30 msimu huu wa Ramadhan, Kila siku, Mdundo.com inatoa fursa ya kipekee kwa waumini wa dini ya Kiislamu kusikiliza na kupakua mpangilio wa muziki maalum wa Kaswida kutoka kwa maDJ mbalimbali kukuza safari yao ya kiroho.” Frida Muraguli, Meneja Miradi wa Mdundo.com nchini Tanzania alitangaza jijini Dar es Salaam leo.

Ofa hii ya kwanza na ya kipekee ipo wazi kwa waumini wa dini zote ikiwemo wapenzi wengine wote wa muziki. Inawawezesha wateja kupata moja kwa moja muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maalum kwa bei nafuu ya TSH 100, TSH 500 au TSH 3,000 – kwa siku, wiki au mwezi kupitia Mdundo.com.

‘Hii ni njia yetu ya kuwatakia ndugu zetu Waislamu Ramadhan Kareem – kwa kuwapa fursa ya kipekee ya kutiririsha, kusikiliza na kupakua muziki wa Kaswida na kupata maudhui mengine ya aina mbali mbali kwa gharama nafuu kupitia huduma yetu bora zaidi ya mziki mtandaoni – Mdundo.com,’ Meneja Masoko wa Afrika Mashariki, William Abagi alithibitisha.

Maudhui husika yanajumuisha aina mbali mbali za muziki ikiwemo Kaswida, Taarab, Singeli, Injili, Bongo, Naija/Afrobeat, Amapiano, Hip hop na nyingine nyingi.

Clouds FM pia wameungana na Mdundo.com kuwapa wasikilizaji muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maarufu wa Clouds FM, ambao sasa unapatikana kupitia ukurasa wa mdundo.com/cloudsfm- https://mdundo.com/a/258048.

Ukuaji wa kasi wa huduma za kutiririsha na kupakua muziki mtandaoni kumeifanya Mdundo.com kuwekeza muda, jitihada na teknologia nyingi zaidi ili kuwainua wasanii wa kiTanzania. Mamilioni ya watumiaji wa mtandao kutoka ndani na nje ya nchi wanatumia huduma hiyo kusikiliza na kupakua muziki wa wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Vile vile, wasanii wengi wa Kitanzania wamechangamkia fursa hii mpya kwa kujisajili na kusambaza maudhui yao kwenye Mdundo.com ili kuwawezesha kuwafikia mamilioni ya wasikilizaji na mashabiki wanaotumia mtandao huu kila mwezi.
MWISHO.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents