Michezo
Mecky Maxime atua Dodoma Jiji

Uongozi wa Dodoma Jiji umefikia makubaliano na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Mecky Maxime kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao. Hatua hiyo inafuatia baada ya Maxime kuachana na Singida BS (zamani Ihefu) kumpisha kocha wa zamani wa Simba na AFC Leopards, Patrick Aussems.
Taarifa ambazo nimezipata kutoka ndani ya uongozi wa Dodoma zilieleza, Maxime amesaini mkataba wa miaka miwili ingawa kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja huku aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Mkenya, Francis Baraza akitimuliwa.