
Kupitia Instagram yake staa huyo wa Singeli nchini ameandika kuwa:
“Nimepata barua ya wito kutoka kwa wasimamizi na walezi wa Sanaa yetu @basata.tanzania ikinitaka kuhudhuria siku ya Kesho na ni kutokana na CHALLENGE ya wimbo wangu mpya wa SHUU ambao nimemshirikisha #BABALEVO & #NTOSHGANZ kutoka Afrika ya kusini maana nilikuwa napambania ndoto yangu ya kuipeleka Singeli kimataifa.
Ni Mara ya kwanza kwangu, kuitwa na @basata.Tanzania hivyo napata mawazo mengi sana, Ninaomba kesho nisindikizwe na Kaka yangu #babalevo Japo ningependa na #ntoshi awepo sema umbali utamzuia.
Mziki ni Marsha yetu, tumetoka hali Duni sana na familia zetu zinapata unafuu kwa kupitia vipaji vyetu, walezi wangu @basata.Tanzania Kijana wenu nitakuja kama barua ilivyonitaka natumai tutakuwa na mazungumzo yakujenga na mwisho NINAOMBA RADHI KWA YEYOTE aliyepata shida/kuudhiwa na challenge ile, naomba mniwie radhi sana KIJANA WENU BADO NAJITAFUTA
Kama hujatazama na kusikiliza audio hii, link hiyo hapo chini