Siku ya leo katika Bandari ya Dar Es Salaam imetua Meli kubwa ya watalii kutoka nchini Norway yenye urefu wa mita 294 sawa na viwanja vitatu vya mpira, imetia nanga na watalii zaidi ya 2,210.
Akiongea na wana habari Mrisho Mrisho Mkurugenzi bandari ya Dar es Salaam amesema kuwa “Meli hii ina uwezo wa kubeba abiria 4,700 na ndio Meli iliyoweka rekodi ya kuwa meli ndefu zaidi kutia nanga katika bandari yetu katika historia ya Tanzania, Tumepokea Meli kubwa ya watalii ina zaidi ya urefu wa mita 250 hii haijawahi kutokea,tumefanya maboresho katika bandari yetu,tumeongeza mlango wa kuingilia meli”
Mbali na hilo Nahodha wa Bandari ya Dar Es Salaam amezungumza pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Utalii nao wakatia neno.