Habari

Meridianbet yafunga safari kuwasaidia walemavu Pwani

Meridianbet Januari 16 2023, ilifunga safari moja kwa moja hadi mkoa wa Pwani wakiambiatana na timu nzima ya Masoko ikiongozwa na Meneja masoko na Mawasiliano Matina Nkurlu kwaajili ya kuwashika mkono wanawake walemavu.

Safari hiyo iliambatana na kutoa vifaa vya elektroniki (Kompyuta) ambayo inaweza kuwasaidia katika matumizi yao ya kila siku ya kuhifadhi data zao muhimu, Vyakula kama Sukari, Unga, mchele pamoja na mafuta ambavyo hivyo vyote vitawasaidia katika matumizi yao ya hapa na pale.

Katika kuwashika mkono Meridianbet iliona kuwa Jukwaa la wanawake na wasichana huko Pwani lilikuwa na uhitaji mkubwa sana wa vitu hivyo ndipo walipoguswa na kuanza safari ya kuelekea katika ofisi yao.

Moja kwa moja walikutana na Mwenyekiti wa jukwaa ambaye ni Mama Happyness ambaye alisema; “Niwashukuru Meridianbet kwa kututembelea na kutuletea vitu kama Mafuta ya kupikia, sukari, Unga, Kompyuta na Mchele ambao utatusaidia kwa mahitaji yetu ya nyumbani”

 Na pia alisisitiza kuwa Meridianbet wakijaliwa kitu warudi tena mahitaji ni mengi sana kwani wanawake na wasichana wenye ulemavu wanamahitaji mengi.

Kwa upande Alfred mdau wa masuala ya kijamii aliipongeza Meridianbet kwa moyo huo wa kujitolea kuwaunga mkono Wanawake na wasichana wenye ulemavu na pia akaiomba kampuni hiyo ambayo mara nyingi hujitolea kwa jamii waendelee na moyo huo wa kuwaunga mkono wenye uhitaji.

Naye meneja wa Masoko na Mawasiliano Meridianbet Martina Mkurlu ameshukuru jukwaa hilo la wanawake na wasichana mkoa wa Pwani kwa kuwapokea vizuri na kuwasihi kuwa vifaa hivyo ambavyo wamepatiwa kama vile kompyuta wavitumie vizuri na wavitunze ili viweze kuwasaidia wao lakini pia na wengine wajao.

Meridianbet inapenda kuushukuru Uongozi wa Jukwaa la Wanawake na Wasichana mkoa wa Pwani kwa kuonyesha ushirikiano mzuri kuanzia mwanzo hadi mwaisho wa zoezi hilo na pia kuwasihi kutunza vifaa hivyo kwa matumizi ya baadae pia. Unaweza kubeti Meridianbet kwa dau dogo la kuanzia TZS 250/= kwa kupiga *149*10#.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents