Habari

Merkel aahidi msaada kwa waathirika wa mafuriko Ujerumani

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema Serikali itashirikiana bega kwa bega na Majimbo ya Magharibi mwa Ujerumani yaliyoathirika kwa mafuriko ili kuzijenga upya maeneo yao.

Akizungumza baada ya kuzuru jana mji wa Schuld, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko, Merkel aliielezea hali katika maeneo hayo kuwa ya kutisha.

Merkel ambaye ameahidi msaada wa haraka wa kifedha, pia alizipongeza juhudi za uokozi zinazoendelea na mshikamano aliyouona wakati wa ziara hiyo, lakini akaonya kwamba shida kwenye eneo hilo hazitotatuliwa haraka.

Kansela Merkel alisema kinachohitajika sasa ni sera inayozingatia maumbile na mabadiliko ya tabia ya nchi kuliko ilivyofanyika katika miaka ya hivi karibuni. Maafa hayo yamesababisha vifo vya watu 160 ikiwa ni 112 katika wilaya ya Ahrweiler iliyoko kwenye jimbo la Rhineland Palatinate. Watu wengine 700 wamejeruhiwa.

Vifo vingine 48 vimeripotiwa katika jimbo jirani la North-Rhine Westphalia.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents