Michezo

Messi hakustaili tuzo ya Ballon d’Or – Toni Kroos, Iker Casillas

Kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos na Iker Casillas wameongoza kwa kukosoa maamuzi yaliyofanywa mpaka kumpatia tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi wakisema hadharani bila kupepesa macho kuwa hakustahili.

Mastaa hao wa soka wamedai kuwa licha ya ubora aliyokuwa nao Messi lakini Robert Lewandowski alistahili zaidi kutokana na uwezo mkubwa aliyoweza kuuonyesha .

Mchezaji huyo wa Paris Saint-Germain amekuwa katika vita kubwa ya ushindani wa tuzo hiyo dhidi ya mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski na kiungo wa Chelsea, Jorginho katika tuzo hizo za Ballon d’Or.

Messi ametwaa taji la Copa America 2021 akiwa na timu yake ya taifa, kinara wa magoli LaLiga kwa msimu wa 2020-21 akifunga mabao 30. Pia nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 ameisaidia Barca kushinda Copa del Rey kabla ya kujiunga na PSG.

Waliyowengi waliamini kuwa, Lewandowski angeweza kuondoka na tuzo hiyo baada ya kuweza ku-maintain kiwango chake cha upachikaji magoli

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland, 33, ameshika nafasi ya pili kwenye tuzo hiyo akiwa amefunga jumla ya magoli 38 kwenye michezo 30 ya Ligi 2021, huku akishinda ubingwa Bundesliga akiwa na Buyern.

Bila kumung’unya maneno mbele vyombo vya habari, Kroos amesema kuwa Messi hakustahili, kwa upande wake Iker Casillas amesema kuwa nyota huyo wa PSG hakustahili.

Je unadhani Messi alistahili tuzo hiyo au Robert Lewandowski  ?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents