
Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi muda wowote huwenda akatua kwenye Klabu ya Al-Hilal inayoshiriki Ligi Kuu nchini Saudi Arabia.
Hayo yana jiri wakati baba mzazi ambaye pia ni wakala wa nyota huyo mzee, Jorge Messi wiki iliyopita ameonekana Saudi Arabia jambo ambalo kama vile amekwenda kuweka mambo sawa.
Kama Messi, atakubali ofa ya pauni miloni 194 kwa mwaka kutoka kwa Al-Hilal hatua hiyo inaweza kumfanya kuwa bilionea.
Mbali na hilo Lionel Messi pia atamzidi mshindani wake Cristiano Ronaldo kuwa mwanasoka anayelipwa pesa nyingi zaidi, wakati Mreno huyo akiwa analipwa pauni milioni 175 kutoka Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia.
Imeandikwa na @fumo255