Burudani

Mfahamu King Sador kutoka Nigeria, msanii anayetabiriwa kuja kufanya makubwa kwenye soko la muziki Afrika (+ Video)

Moja ya taifa lililojaliwa wasanii wengi ni Nigeria, huyu anaitwa King Sador ni msanii wa muziki wa pop wa kutoka nchini Nigeria, anayeishi Afrika Kusini.

Inelezwa kuwa King ni mmoja ya wasanii walifanikiwa kupata elimu ya darasani kwani ni mhitimu wa kompyuta ya mkononi kutoka Chuo Kikuu nchini Malaysia, alianza rasmi kazi yake ya muziki mwaka 2013 alipohitimu elimu yake ya chuo.

Kama inavyofahamika kuwa wasanii wengi vipaji vyao vilianza kuonekana kwenye nyumba za ibada mfano misikitini kwa kuimba Qaswida unaambiwa King Sador Kipaji cha muziki kilianza kuonekana akiwa katika kwaya ya kanisani. 2020  aliachia albamu ya GODs PLAN, yenye nyimbo 16.

Hivi karibuni msanii huyu aliachia kazi yake mpya yenye jina la Connect iliyotengenezwa na mtayarishaji wetu wa Afrika Kusini Skhumba De Dj ambayo pia ilimshirikisha mwimbaji wa kike wa Afrika Kusini Casey Leona na msanii wa Kitanzania Sam P akiwa na baadhi ya wasanii wa saxophonist kujisikia kutoka SammySax.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents