Fahamu

Mfahamu mwanafunzi aliyetatua fumbo la Hesabati la miaka 50 ndani ya wiki moja, wakali wa ‘Mathematics’ hawaamini

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu nchini Marekani ametatua hesabu ya miaka 50 katika muda wake wa ziada , chini ya kipindi cha wiki moja.

Lisa Piccirillo alikuwa anafanyia kazi shahada yake ya udaktari katika chuo kikuu cha Texas , wakati alipotatua fumbo hilo la Conway.

Alianza kupiga kelele, kwanini hufurahii?”,Piccirillo aliambia tovuti ya habari ya Quanta.

Tatizo hilo la hesabu la Conway lilipendekezwa na mwanahesabati wa Uingereza John Horton Conway 1970, lakini bi Piccirillo alilisikia kwa mara ya kwanza katika warsha moja mwaka 2018.

”Sidhani alikuwa amefahamu kwamba hesabu hiyo ilikuwa maarufu sana zamani”, alisema Profesa Gordon.A nautical knot

Fundo la hisabati

Kazi ya Bi Piccirillo ilichapishwa mapema mwaka huu na jarida la hesabati la Annals Mathematics na tangu alipotatua hesabu hiyo amefanywa kuwa naibu profesa katika taasisi ya teknolojia ya Massachusetts MIT.

Fumbo hilo la Conyway lilikuwa halijatatuliwa kwa muda mrefu na wanahesabati wengi werevu walijaribu kulifumbua lakini wakashindwa, kulingana na Javiwe Aramayona, mtafiti katika chuo kikuu cha Madrid na mwanachama wa taasisi ya hesabati ya Uhispania ICMAT.

Topology ni muhimu katika sekta nyingi za sayansi na imetumika na wanasayansi kutafiti tabia za vitu katika masoko tofauti na maumbile ya molekyuli za jeni.The Conway knot

TFumbo hilo la Conyway lilikuwa halijatatuliwa kwa muda mrefu

Je fumbo la hesabu ni lipi?

Mafumbo ya hesababti ndio chanzo cha tawi maalum la hesabati kwa jina Topology.

Kwa maana rahisi , topology ni utafiti kuhusu tabia za vitu huku vikiundwa , kukunjwa na kuvutwa bila kuvunjika.

Fumbo hilo la Knot ni mojawapo ya tawi la topology.

Mbali na mifano mingine, mwisho wa fumbo hilo huwa umeshikana – mfano wake ni umbo la mviringo – ambalo haliwezi kufunguliwa.

Lakini huwa ngumu kwa kuwa fundo hilo lina maeneo mengi ambapo linapishana.

”Lengo la wazo hilo ni kufikiria kamba” , anasema Marithania Silvero, kutoka taasisi ya hesabati ya chuo kikuu cha Seville.

”Nadharia za fundo hutafiti uharibifu unaoweza kufanywa katika kamba” , anaongezea.

”Kwa maana nyengine ni kwamba, tunaangazia jinsi tunavyoweza kuikunja kamba hiyo”, kuivuta na kuikamua. Kile ambacho hatuwezi kukifanya ni kuikata kamba hiyo. Hilo linakatazwa”.Table of knots

Sawa na uhalisia wa maisha, ugumu wa hesabati pia huweza kutofautiana

Topology ni muhimu katika sekta nyingi za sayansi na imetumika na wanasayansi kutafiti tabia za vitu katika masoko tofauti na maumbile ya molekyuli za jeni.

Fundo la Conyway

Mtu aliyevumbua fundo hilo la kamba , John Horton Conway alifariki Aprili na Covid-19 akiwa na umri wa miaka 82.

Msomi huyo ambaye ni mzaliwa wa eneo la Liverpool ni mtaalam wa muda mrefu, mwenye ushawishi wa hisabati na ambaye alifanya kazi katika vyuo vikuu vya kifahari kama vile Cambridge na Princeton.

Alikuwa “mtu aliyependwa zaidi ulimwenguni”, kulingana na mwandishi wa biografia, Siobhan Roberts.

Alielezewa kama “Archimedes, Mick Jagger, Salvador DalĂ­ na Richard Feynman wakikusanywa na kuwa mtu mmoja.”John Horton Conway

John Horton Conway alifariki kutokana na Covid-19 mwezi Aprili

Lakini, mwanafunzi aliyehitimu aliwezaje kutatua shida ya fundo maarufu kwa haraka?

Bi Piccirillo alitatua fundo la Conway, ambalo lina misalaba 11 au mikunjo, kwa kutengeneza toleo linalofanana na hilo, linalojulikana kama “fundo la ndugu”, ambalo lilithibitisha kuwa rahisi kidogo kujifunza.

Kwa kutengeneza fundo hilo, na kulitatua aliweza kutumia matokeo yake kutatua fundo la Conway.

“Sikujiruhusu kulitatua fundo hilo wakati wa mchana kwa sababu sikuona kuwa ni hesabu halisi,” aliiambia gazeti la Quanta.

“Nilidhani ilikuwa, kama, kazi yangu ya nyumbani. Kwa hivyo nilienda nyumbani tu na kuifanya.”MIT building

Ms Piccirillo kwa sasa anafanya kazi katika taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts

Bi Piccirillo alizaliwa katika eneo la mashambani zaidi nchini Marekani la Maine na alijifunza hesabati katika chuo cha Boston College.

”Mwaka 2013, nikiwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza , alijishindia ufadhili wa kuendelea kusoma zaidi katika wakfu wa kitaifa wa sayansi”.

”Alipoanza, hakuwa na elimu yoyote ya msingi katika nadharia ya mafundo wala mafunzo yoyote zaidi ya hesabu za algebra,” alisema Elisenda Grigbsy”, mmoja wa walimu wa Bi Piccirillo, akizungumza na gazeti la Chuo cha Boston.

”lakini ndani ya wiki moja , alifanikiwa kutatua hesabu ambazo zilikuwa zikiwapatia tabu wanafunzi wengine”.

Ufanisi wa Bi Picirillo kufungua fundo hilo la Conway unaweza kuwapatia moyo wanawake zaidi kuchukua kazi za hesabati ambapo kuna pengo kubwa la usawa wa kijinsia.

Takwimu za idara ya leba nchini Marekani zinaonesha kwamba wanawake wanawakilisha asilimia 26 ya watu wanaofanya kazi ”katika tarakilishi na hesabati” nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents