Fahamu

Mfahamu Mwanasheria mkuu wa kwanza Kenya aliyefariki dunia, Charles Njonjo

Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Kenya aliyekaa ofisini kuanzia 1963 hadi 1979, Charles Mugane Njonjo, amefariki Dunia leo Jumapili Januari 2, 2022 akiwa na miaka 101.

Familia yake imesema amefariki akiwa nyumbani kwake Muthaiga Nairobi, baada ya kusumbuliwa na Nimonia.

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba asubuhi ya leo, Jumapili tarehe 2 Januari 2022, nimepokea taarifa za kuhuzunisha za kufariki kwa Charles Mugane Njonjo,” – Rais Uhuru Kenyatta akitangaza kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe Charles Mugane Njonjo.

Charles Mugane Njonjo alistaafu kama mwanasheria mkuu akiwa na umri wa miaka 60.

Baadaye Njonjo alichaguliwa bila kupingwa katika Bunge la Kitaifa Aprili 1980 kama Mbunge wa Jimbo la Kikuyu.

Aliyekuwa rais Hayati Daniel Moi alimteua katika Baraza la Mawaziri mnamo Juni 1980 kuhudumu kama Waziri wa Masuala ya Ndani na Kikatiba.

Kufariki kwa Mhe. Njonjo ni pigo kubwa sio tu kwa familia yake bali kwa Wakenya wote na kwa hakika, bara zima la Afrika kwa sababu ya jukumu lake kuu katika kuanzishwa kwa taifa la Kenya wakati wa uhuru,” Rais alisema.

keny

Taarifa kutoka kwa familia zinasema, maiti ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Charles Njonjo tayari imechomwa katika mji wa Kariokor jijini Nairobi.

Charles Mugane Njonjo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mzaliwa wa Kenya kati ya 1963 na 1979.

Alistaafu kama mwanasheria mkuu akiwa na umri wa miaka 60.

Baadaye Njonjo alichaguliwa bila kupingwa katika Bunge la Kitaifa Aprili 1980 kama Mbunge wa Jimbo la Kikuyu.

Aliyekuwa rais Hayati Daniel Moi alimteua katika Baraza la Mawaziri mnamo Juni 1980 kuhudumu kama Waziri wa masuala ya ndani na Kikatiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents