Habari

Mfanyabiashara kutoka Rwanda apigwa risasi na kuuawa Msumbiji

Mfanyabiashara raia wa Rwanda amepigwa risasi na kuuawa katika mainspaa ya Matola ,kilomita chache kutoka mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.

Levocat Karemangingo alipigwa risasi karibu mita 50 kutoka kwenye makazi yake yaliyopo katika makazi ya Liberdade Jumatatu asubuhi.

Imedaiwa kuwa uhqalifu huo ulifanywa na majambazi waliokuwa katika magari matatu ambao walilizuwia gari lake kabla ya kummiminia risasi.

Wauaji hao hadi sasa hawajulikana, jambo lililoitikisa jamii ya Wanyarwanda wanaoishi Msumbiji.

Polisi walikuwa kwenye eneo la tukio kufanya uchunguzi wa mwili wake na mwili wake ulipelekwa kwenye hospitali ya jimbo.

Baadhi ya Wanyarwanda wamewaambia waandishi wa habari kuwa uhalifu huo uliwalenga raia wanaopinga serikali ya sasa ya Rwanda na kudai kuwa watu wengi wanalengwa.

Wanyarwanda walioko Msumbiji wameiomba serikali kuwapatia ulinzi zaidi.

Mwaka 2019, Mnyarwanda mwingine, Louis Baziga, aliuawa kwa risasi katika kitongoji cha Maputo baada ya watu wenye gari kuzuia gari lao. Alifahamika kuunga mkono serikali ya Rwanda.

Related Articles

Back to top button