Siasa

Mfumo wa anwani za makazi ni endelevu – Dkt. Jim Yonazi 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amesema utekelezaji mfumo wa anwani za Makazi ni zoezi endelevu na halina mwisho kwani wananchi wanajenga na Tanzania inaendelea kukua kila siku.


Dkt. Yonazi ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa upatikanaji huduma za Mawasiliano na utekelezaji wa Operesheni anwani za Makazi katika makazi mapya ya wafugaji na wakulima wa Kijiji cha Msomera kilichopo Kata ya Misima, Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga

Amesema kuwa, yupo katika Kijiji hicho cha Msomera na amefurahi kuona nyumba zimewekewa namba na kunaendelea kuhakikisha kwamba kila mtu anapata anwani ya Makazi yake, lakini pia zoezi hilo ni endelevu na halina mwisho kwa sababu nchi bado inajengwa na shughuli mbalimbali za maendeleo zinakua kila uchwao.

Ameongeza kuwa kutokana na zoezi hilo kila mtu atajulikana kwa maana sasa ana fursa ya kushiriki katika uchumi wa eneo lake, uchumi wa kitaifa na uchumi wa kimataifa wa Dunia nzima kwa mana kwamba anaweza kupata kiurahisi huduma kama za afya, Polisi, Zimamoto kwa kujulikana anapoishi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents