Habari

Mgogoro wa kiuchumi Ujerumani, raia watakiwa kuwa wamoja

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa wito kwa umma kukabiliana kwa pamoja na matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo wakati kukishuhudiwa mfumuko mkubwa wa bei.

Kansela Scholz ametoa rai hiyo siku chache baada ya takwimu kuonyesha kwamba bei za bidhaa nchini Ujerumani zilipanda kwa asilimia 7.6 mwezi Juni ukilinganisha na mwaka uliopita.

Scholz anatarajiwa kufanya mazungumzo na vyama vya wafanyakazi na waajiri kuona jinsi gani ya kushughulikia kupanda maradufu kwa gharama za maisha.

Wachumi na wanasiasa wametoa maoni kadhaa katika siku za hivi karibuni ili kupunguza mzigo kwenye bajeti za kibinafsi.

Ofisi ya Kansela imesema kuwa inakusudia kutafuta njia mbadala ya nyongeza zaidi ya mishahara wakati wa mazungumzo na vyama vya wafanyakazi. Lakini kuna hofu kwamba hatua hiyo inaweza kuchochea mfumuko zaidi wa bei.

Related Articles

Back to top button