Habari

Mgumba ajutia jaribio la kuiba mtoto Muhimbili, asimulia A-Z (Video)

Ni tukio la kweli ambalo lilitokea miaka 7 iliyopita baada ya Shamila Makwenjula (50) kudai kupokea kipigo na manyanyaso ya kila siku kutoka kwa mume wake baada ya kushindwa kupata mtoto.

Bongo5 kupitia TheDark imefanya mahojiano mwanamke huyo ambaye aliachika katika ndoa yake baada ya miaka kumi bila kupata mtoto.

Shamila ambaye amekuja na Chama Cha Wagumba kwaajili ya kupaza sauti na kueleza jinsi wanavyonyanyasika, akilia kwa uchungu kueeleza jinsi alivyotua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwaaajili ya kuiba mtoto, amedai wagumba wanapigia wakati mgumu sana kwa jamii za Watanzania.

Amedai alifikia hatua ya kwenda Hospitali ya Muhimbili kwaajili ya kuiba mtoto ambapo amesimulia kisa hicho A-Z.

Amedai wameamua kujitokeza hadharani kupaza sauti kwa Watanzania waelewe manyanyaso wanayopitia hali ambayo inawafanya waathirike kisaikolojia na kuwa tayari kufanya lolote kama alivyofanya jaribio la kuimba mtoto.

Amedia katika kuangaika kwake kutafuta mtoto, kuna dawa za mitishamba ambayo aliambiwa akaitumie kwa kuila na chakula katikati ya shimo la choo na mabaki atumbukize choooni.

Kwa sasa Shamila anaishukuru serikali kupitia Waziri wa Maendeleo ya Jamii @gwajima kwa kusikia kilio chao na kusajili chama chao huku wakiwataka Watanzania kuacha kuwanyanyasa wagumba kwani hawajataka kuwa hivyo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents