Habari

Mhandisi Kundo: Marufuku kumsainisha mwananchi mkataba kwa lugha za kigeni

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew, amepiga marufuku kumsainisha mwananchi mkataba kwa lugha za kigeni kwani yeyote anayefanya hivyo atakuwa na dhamira ovu dhidi ya mwananchi ndio maana anasainishwa mkataba kwa lugha asiyo ifahamu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akizungumza na watendaji wa TTCL kuhusu usambazaji wa huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Wilayani Mkinga.

Mhe. Kundo amesema hayo katika ziara yake ya kukagua ujenzi, uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano, Wilayani Muheza Mkoani Tanga na kusema kuwa Serikali itasimamia haki na maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha wanasainishwa mikataba kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili mwananchi kusaini kitu anachokielewa na kulipwa fedha kulingana na ukubwa wa maeneo wanayoyatoa kwa ajili ya ujenzi wa minara ya mawasiliano.

Amesema kuwa dhamira ya Wizara hiyo ni kuondoa migogoro ndani ya Sekta ya Mawasiliano kwa watoa huduma kufuata taratibu wakati wa ujenzi wa minara ikiwa ni pamoja na kupata vibali vinavyohitajika na kusaini mikataba na Serikali za vijiji kwa ajili ya ulinzi wa minara ya mawasiliano.

Aidha, Mhandisi Kundo alitoa maagizo kwa watoa huduma kufanya malipo kupitia akaunti za benki kutoka kwenye kampuni kwenda moja kwa moja kwa walioingia nao mkataba ambao ni wamiliki wa maeneo waliyojenga minara ili kampuni kujiridhisha inamlipa mhusika na sio
Vinginevyo.

Sambamba na hilo Mhe. Kundo alielekeza taasisi mbili za mawasiliano ambazo ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuhakikisha wanakuja na majibu ya kupata suluhisho la kudumu tatizo la muingiliano wa mawasiliano katika maeneo yote ya mipaka nchini ifikapo tarehe 16/08/ 2021.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents