Mihayo: Akili mnemba mimi naiita ‘akili kasuku’
Makamu Rais na Meneja Mikakati wa Kampuni ya Airpay Tanzania, Mihayo Wilmore amesema kuwa Akili Mnemba (AI) yeye anaweza kuhiita akili kasuku kwani ndege huyu ufanya kile anachoambiwa au kuamrishwa kama ilivyo AI.
Mihayo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wakurugenzi na viongozi wa taasisi mbalimbali lililojadili uongozi katika zama za akili mnemba, kusimamia furs ana changamoto katika mabadiliko ya kidigitali Tanzania.
“AI inasaidia pale ambapo unataka kubadilisha mfumo wako wa kila siku kwa kuielekeza nini ifanye, mimi naweza kuiita AI akili kasuku, maana kasuku unachomwambia ndicho anafanya kama ilivyo kwa AI,” amesema
Hata hivyo amesema bado Tanzania hatujaweza kutengeneza AI za kwetu kwani nyingi zinazotumika ni za mataifa ya nje na kwamba ni muhimu kuwa na mikakati thabiti itakayowezesha utumiaji wa teknolojia hiyo nchini uendane na mazingira halisi kwa kuzingatia tahadhari muhimu.