HabariSiasa

Miili ya watoto ilivyofunikwa na vifusi Gaza, hakuna wa kuwaokoa

Ikiwa bado tunaendelea kukufahamisha yanayoendelea huko Israel na Gaza, Adnan Al-Barash, mwandishi wa habari wa BBC, Khan Yunis amezungumza na wenyeji.

Mmoja amesema mwendelezo wa mashambulizi makali ya anga katika Ukanda wa Gaza kwa kama saa moja umetokea katika eneo la Nuseirat na kambini, ambayo iko katikati ya Ukanda wa Gaza.

Anasema, nyumba moja iliyokuwa inahifadhi watu kadhaa waliokimbia makazi yao ilishambuliwa kwa bomu.

Mashambulizi hayo yanasemekana kusababisha vifo vya takriban watu 10 na majeruhi kadhaa.

Idadi ya nyumba zililengwa huko Rafah, Deir Al-Balah, katika eneo la Tal Al-Hawa, na Mtaa wa Al-Nafaq, yote ambayo yalisababisha mauaji ya makumi.

Takriban watu 350 waliuawa ndani ya saa 24 huku karibu 1,500 wakijeruhiwa.

Watu wengi bado wako chini ya vifusi, na baadhi walioshuhudia wanasema, ‘’Tunasikia mayowe kutoka chini ya ardhi,’’ kutokana na kushindwa kuopoa miili na majeruhi kwasababu ya uwezo na vifaa vinavyohusiana na shughuli za uokoaji wa raia.

‘’Hakuweza kufanya kazi yake kutokana na uhaba mkubwa wa wafanyakazi, zana na vifaa,’’ shuhuda mmoja alisema.

Wizara ya Afya huko Gaza inakabiliwa na uhaba mkubwa na iko chini ya tishio kutoka kwa jeshi la Israeli ikiwa itahamisha makao yake makuu kaskazini mwa Gaza italipuliwa na ndege, Wizara ya Afya ilisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents