Habari

Mikopo Kausha Damu yapata suluhu Gairo

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame ameitisha Mkutano wa Wadau wa Sekta Ndogo ya Fedha kujadili changamoto za Utendaji Kazi wa Taasisi ndogo za Fedha Wilaya ya Gairo.

Mkutano huu uliitishwa kufuatia Uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Gairo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na Watumishi ambao wamekuwa wakichukua Mikopo kutoka Taasisi hizo. Baadhi ya kasoro zilizobainika ni baadhi ya Taasisi kufanya kazi bila kuwa na leseni kutoka Taasisi zinazosimamia Sekta ya Fedha ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Tume ya Ushindani (FCC) na BRELA, Kukwepa kulipa ushuru wa Halmashauri, Mikataba kandamizi kwa wateja, baadhi ya Taasisi kuchukua kadi za Benki za wateja na namba za Siri kinyume na Sheria, kuwa na Watumishi wasiokuwa na sifa, Riba kubwa kinyume na maelekezo ya BOT nk.

Kufuatia Dosari hizi Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame, alieleza Serikali ingependa kuona Taasisi hizi zinakuwa ili ziendelee kuchangia ukuaji wa uchumi na kutoa ajira, hivi Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan imejikita katika kuilea Sekta Binafsi ili iweze kukua.

Hivyo, amezitaka taasisi zote kurekebisha dosari mbalimbali zilizobainika. Aidha, ametoa mwezi Mmoja kwa Taasisi zote kuhakikisha zinakidhi vigezo vyote vilivyoelekezo kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuwa na leseni za BOT, FCC na BRELA, kurejesha kadi za Benki kwa wateja wao, kurekebisha Mikataba ya wateja wao na kuhakikisha Mikataba hiyo inakidhi vigezo vilivyowekwa na FCC, kulipa ushuru wa Halmashauri ulikwepwa, kurejesha fedha za wateja ambao zilichukuliwa kama marejesho kinyumbe na utaratibu.

Mkutano huu ulihudhuriwa na wataalamu kutoka BOT ambao walimwakilisha Gavana wa Benki KUU, Wataalamu kutoka Tume ya Ushindani (FCC), Maafisa wa TRA, BRELA, Taasisi za Fedha 25 zilizopo Wilaya ya Gairo, wawakilishi wa Vyama vya wafanyakazi, Viongozi wa Sekta Binafsi, vyombo vya Ulinzi na Usalama na viongozi wa wananchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents