Burudani

Milioni 9 zamtenga Gigy Money na mwanae siku 30

Msanii wa muziki wa Bongo Flava na video vixen, Gigy Money amesema kutokana na utafutaji mara nyingi analazimika kutengana na mwanae.

Muimbaji huyo katika mahojiano na XXL ya Clouds Fm amesema ni vigumu yeye kulala nyumbani wakati hana fedha.

“Nilienda Nairobi nikakaa mwezi mzima na nilimuacha mtoto na mama yangu, hakuna mtu anaweza kuacha dola 4,000 (sawa Tsh. Milioni 9) kirahisi,” amesema Gigy Money.

Ameendelea kwa kusema analazimika kufanya hivyo kutokana anategemewa na familia yake. Gigy Money ni mama wa mtoto mmoja wa kike itwaye Mayra.

Related Articles

Back to top button