Burudani

Mimi Mars alikimbia beef la Vera Sidika na Hamisa Mobetto

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Mimi Mirs amekataa katu kuzungumzia kile kinachoendelea kati ya Vera Sidika na Hamisa Mobetto.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na ngoma yake ‘Dedee’, alipoulizwa na kipindi cha Clouds E kuhusu beef ya video vixen hao alijibu;.

“Tangia nimeacha kufuatilia haya mambo siyo kivile kwa hiyo sina comment kuhusiana na hawa watu, siwezi kusema chochote kila mtu anatafuta kwa jinsi yake, labda wao ndio jinsi wameona” amesema Mimi Mars.

Mimi Mars alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Weekend Gossip ambacho kinaruka kupitia TV1 ambacho kilikuwa kinahusika na udaku wa mastaa mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents