Burudani

Mimi si shabiki wa Vanessa Mdee – Baby Madaha

Msanii wa muziki ambaye ni zao la shindano la kusaka vipaji BSS, Baby Madaha amedai kuwa Vanessa Mdee si msanii mkali kama baadhi ya watu wanavyosema.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kwamba yeye anaamini kuna wasanii wakali zaidi yake lakini hawapewi nafasi wanayostahili kama anayopewa muimbaji huyo anayechanja mbuga zaidi kimataifa.

“Mimi si shabiki wa Vanessa hata muziki wake, hata nyimbo zake sizisikilizi kabasa,” alisema Baby Madaha. “Kuna wasanii wakali hawapewi tu nafasi, mimi ni shabiki wa Lady Jaydee, akina Mwasiti kuna wasanii wengi wanafanya muziki nzuri,”

Madaha amedai hamuonei wivu Vanessa Mdee kutokana na mashavu anayopata ila kuna baadhi ya sifa anapata ambazo sio saizi yake.

Muimbaji huyo ambaye anajipanga kuachia wimbo mpya hivi karibuni amekaa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents