Michezo

Mino Raiola ‘aibuka’ Hospitali, ashangazwa na taarifa za kifo chake

Wakala Mino Raiola aibuka akiwa kitandani Hospitali na kukanusha taarifa za kifo chake ambazo zimeonekana kuenea kwenye vyombo mbali mbali vya habari.

”Hali ya afya ya sasa kwa wale wanaoshangaa: Nikichukizwa mara ya pili katika miezi 4 wananiua. Inaonekana pia kuwa na uwezo wa kufufua,”- Mino Raiola

Raiola ameonekana kukanusha taarifa hizo kwa ujumbe wake wenye kujaa hasira, kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa twitter.

Mapema taarifa kupitia mitandao mikubwa ya michezo barani Ulaya iliandika taarifa za kifo cha wakala huyo mashuhuri Ulimwenguni.

Ujumbe wa Real Madrid ukionesha kuuzunishwa na taarifa za kifo za Raiola kabla ya mwenyewe kujitokeza hadharani na kukanusha.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button