Habari

Miradi ya zaidi ya Bilioni 1, kuchunguzwa na TAKUKURU Singida

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imechunguza miradi ya maendeleo yenye thamani ya  zaidi ya Sh. 1. Bilioni ili kuona utekelezaji wake ulikwenda kama ilivyopangwa na  kama hauna viashiria vya ubadhilifu.

Hayo yamesemwa  na Mkuu wa TAKUKURU, Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Taasisi katika kipindi cha robo ya nne ya mwakawa fedha 2020/2021.

Alitaja miradi ilichunguzwa kuwa ni Afya,ambapo kulikuwa na  jumla ya miradi  Saba yenye thamani ya Sh. 820,000,000,  Elimu miradi iliyopitiwa miwili yenye thamani ya Sh. 70,000,000, Ujenzi wa Majengo ya Halmashauri mradi mmoja wenye thamani ya Sh. 600,000,000 na mradi wa Ujenzi wa Barabara mmoja wenye thamani ya Shilingi za kitanzania 160,530,000.

Alisema thamani ya miradi hiyo ni Sh. 1,650,530,000 ambayo ni  kwa mujibu wa fedha zilizoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi husika ya maendeleo.

” Kwa ujumla yaliyobainika wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo ni ukiukwaji wa taratibu za manunuzi kwenye baadhi ya miradi, kukosa ushirikiano wa nguvu za wananchi, ucheleweshaji wa fedha kwenye vituo kutoka Halmashauri na changamoto wakati wa utekelezaji wa sheria mpya inayoelekeza manunuzi ya vifaa kwa wazabuni waliosajiliwa  na GPSA ambao wengi wao gharama zao zipo juu na hivyo kusababisha miradi kutokamilika,” allisema Widege.

Katika hatua nyingine taasisi hiyoimetangaza kuwachukulia hatua kali  wote watakao bainika wanatumia nembo nembo ya taasisi kwa vitendo idegevya uhalifu.

” Takukuru inazidi kutoa rai kwa wanan wote kuwa kumekuwepo na wimbi la matapeli ambao wanajifanya ni maafisa wetu, wamekuwa wakipiga simu kwa wananchi na kuwatisha kuwa wanaitwa kwenye ofisi zetu na kuwa wanatuhuma za rushwa jambo ambalo sio la kweli,” alisema.

Hata hivyo Widege alitoa onyo kali kwa watu hao aliowaita matapeli kuacha mara moja vitendo hivyo na endapo watakaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents