Misri yawaachia huru Wanaharakati waliokuwa kizuizini

Misri jana imewaachilia huru wanaharakati sita akiwemo mwandishi habari Bi.Esraa Abdel-Fattah, ambaye alikuwa akitazamwa kama mchochezi mkuu wa vuguvugu la umma la mwaka 2011. Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Marekani kuionya Misri kuhusu ukandamizaji wa wanaharakati wa haki za binaadamu nchini humo.

Tangu Rais Abdel-Fattah al-Sisi achukue madaraka mwaka 2014, Mkuu huyo wa zamani wa jeshi ameongoza ukandamizaji mkubwa wa wapinzani.

Wachambuzi wanasema hatua hiyo ya  Serikali inalenga kupunguza shinikizo la Kimataifa kuhusu rekodi ya Misri ya Haki za binaadamu. Mwendesha mashitaka aliamuru kuwachiwa Abdel-Fattah baada ya miezi 22 akiwa kizuizuni kabla ya kesi. Aliachiwa pamoja na Abdel Nasser Ismail, kiongozi wa chama cha Popular Alliance, na Gamal El-Gammal, mwandishi habari na kiongozi wa upinzani.

Aidha, mwanasheria maarufu na mwanaharakati wa haki Mahienour El-Masri na waandishi wa habari Motaz Wadnan na Mostafa El-Asar waliachiwa huru.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button