Mrembo @official_lindasamson ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kupitia kampuni yake ya We Planners amekuja na Miss Dar Zone ambapo usaili wake utafanyika weekend hii.
Akiongea na Bongo5 Onomo Hotel Jumamosi hii jijini Dar Es Salaam kuhusu tasnia ya urembo na jinsi watu wanavyoichukulia, Linda amedai watu wangi wamekuwa wakisikia mabaya mengi yanayofanywa na baadhi yao kuliko mazuri.
Alisema kuna warembo wengi wanafanya mambo makubwa lakini hawasikiki kuliko yale mabaya yanayofanya na wachache.
Amemtaja Jokate, Basila Mwanukuzi pamoja na wengine kama mfano wa kuigwa katika tasnia hiyo.