Mister Joozey sukari ya warembo

Kwa melody za juu na za chini utamu wa muziki mzuri huwezi acha kumzungumzia DJ
@misterjoozey ambapo katika tasnia ya kucheza na santuri kwenye 1 na 2 Joozey amekuwa mwenye upekee sana licha ya kutumbuiza na wasanii wakubwa wa Kimataifa akiwemo Burnaboy,Rema,Fireboy, na wengine wengi joozey amefanikiwa kuiteka burudani ya Masaki na hii ni lile vibe lake la kupiga mziki usiku mzito huku wengi wakimsifia kwenye mixing kali za amapiano na Afro House
Licha ya kuwa na kipaji cha kutengeneza mziki ikiwemo wimbo na Tobesta,Namficha aliyofanya na Harmonize Joozey ameonekana ni mwenye kuandamwa sana na hii ni kutokana na picha za kimitego ambazo zimeonekana zikisambaa hivi karibuni bado wengi wanajiuliza Mwamba anatoka na nani?? licha ya kumposti mtoto wake siku za hivi karibuni