Tangu kuvuja kwa taarifa kuwa Lionel Messi ndiye mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka huu kumekuwa na mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ya nani ndiyo angestahili kuchukua.
Messi anapewa nafasi ya kuchukua Ballon d’Or kwa mara ya nane kutokana na kuipatia Ubingwa wa Kombe la Dunia timu yake ya taifa ya Argentina mwezi Disemba pale Qatar huku akibeba na Golden Ball kwa kufunga goli saba.
Na wanaompa nafasi Erling Haaland ni kutokana na Kuvunja rekodi kadhaa akiwa mwenye mafanikio ndani ya Manchester City ikiwa ni sanjari na kufunga magoli mengi zaidi ndani ya msimu mmoja tu wa Premier League bao 36. Na 16 kwenye mashindano yote aliyopata kushiriki huku akimaliza na Ubingwa wa UEFA Champions League mwezi Juni.
Messi amefanya vizuri kwenye Kombe la Dunia wakati Haaland akifanya powa ngazi ya Klabu, kuvuja kwa taarifa kuwa Mwamba huyo wa Argentina ndiye mshindi hatakabla hajatangazwa kumezua mijadala.
Pep Guardiola kwa upande wake amesema wote wawili wanastahili na yeyote atakayeshinda hatasema mmoja hajatendewa haki.
Je, Nani anastahili kushinda Ballon d’Or..?
Imeandika @fumo255