Habari

Mjukuu akuta Lamborghini na Ferrari kwenye gereji ya bibi yake baada kupita zaidi ya miongo miwili

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Eriegin amesema kuwa katika hali isiyo ya kawaida amefanikiwa kuyaona magari mawili ya kifahari ya Lamborghini Countach na Ferrari 308 kwenye gereji ya bibi yake baada ya kupita zaidi ya miongo miwili toka kufariki kwake.

Mjuku huyo ambaye ni mwanafunzi ameyasema hayo huku akiposti picha za magari hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Reddit nchini Marekani na kuzua gumzo kubwa katika baadhi ya vyombo vya habari.

Kijana huyo alivunja na kuingia ndani ya gereji hiyo ambayo iliachwa kutumika kwa kipindi kirefu na kukuta magari hayo Lamborghini Countach  aina ya silva na Ferrari 308 nyekundu yenye thamani ya pauni 430,000.

“Babu yangu aliyanunua magari haya mwaka 1989 kwaajili ya kumsaidia katika biashara zake lakini kutokana na kupandishiwa bima kwa muda huo alishindwa kuendelea kuendeleza kampuni yake na hivyo kupelekea kuhifadhiwa kwenye gereji kwa kipindi chote hicho cha zaidi ya miaka 20,”amesema kijana huyo aliyetumia jina la Eriegin.

Mamia ya watu kwenye mtandao huo wa kijamii walikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu wengine wakiuliza kwa nini yalikuwa hapo muda wote na hata wengine kufika mbali zaidi kwa kuhitaji kuuziwa magari hayo kutoka kwa kijana hiyo.

Wakati kijana huyo akisema kuwa amefurahi mno kupata magari hayo licha ya kumkumbusha machungu ya wazee wake na kuongeza amejiskia vibaya kutokana na kuwa magari hayo yalikuwa yamefichwa kwa kipindi chote hicho na kuahidi yatakuja kusaidia familia mara baada ya kukamilika marekebisho yake.

Related Articles

19 Comments

  1. Fedo Mathube Jr., tatizo ni kwamba, yeye akiona gari ya staili fulani imeingia nchini kwetu na yeye anajua kua ndio ya mwaka huo, kumbe ina miaka kama kumi naa… Kwa mfano sa hiv unaeza nunua gari ilotoka 2002 lkn kwa huku ndio iko sokoni

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents