Habari

Mjumbe wa EU aiomba radhi Liberia kwa kusema mji mkuu wake mchafu kuliko yote Afrika

Mkuu wa Umoja wa Ulaya nchini Liberia ameomba radhi kwa kusema mji mkuu wa Liberia, Monrovia ni mchafu sana na hivyo kurudisha nyuma maendeleo.

Laurent Delahousse alisema alitoa maoni hayo akikusudia kuwapa muamko wakazi wa mji huo kubadilika katika mazoea yao ya kutupa taka hovyo na kuboresha usimamizi wa kuweka mazingira kuwa safi kwa kuwa wanapokea ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa mjini Monrovia, alisema “Monrovia ni mji mchafu sana”.

“Katika miji yote mikuu ya Afrika ambayo nimewahi kuiona awali, sijawahi kuona mji mkuu mchafu kama huu,”aliongeza.

Bwana Delahousse alifafanua maoni aliyotoa kuwa yalikuwa na nia ya kila mtu kuwajibika kutunza uzuri wa mji huo na sio kumkashifu au kumdharau mtu yeyote katika mji mkuu wa Liberia.”

Ameomba radhi kwa serikali na yeyote aliyejihisi kukashifiwa kwa ujumbe wake ambao haukueleweka vizuri.

Aidha watu wengi bado wanaona kuwa ujumbe wake ulikuwa na ukweli juu ya hali ya mji mkuu wa Liberia.

Related Articles

Back to top button