Habari

Mjusi aliyesafiri umbali wa maili 4,000 apatikana kwenye nguo ya ndani

Mjusi anayependa nguo za ndani amepatikana kwenye sidiria baada ya kusafiri kutoka Barbados hadi Yorkshire kwa ndege.

Mjusi mdogo, ambaye sasa anaitwa Barbie, aligundulika na Lisa Russell wakati akifunua mkoba wake baada ya kufika nyumbani kwake karibu na Rotherham, South Yorkshire.

Bi Russell alisema: “aliposogea, nilianza kupiga kelele. Sio kile unatarajia kukiona kwenye sidiria yako baada ya safari ya maili 4,000.” Barbie sasa yuko salama katika uangalizi wa kituo cha uokozi na uangalizi wa wanyama, RSPCA.

Mwanamke huyo anayeishi Thrybergh, alifika nyumbani kwake Jumanne na kuanza kufungua sanduku lake baada ya likizo katika visiwa vya Caribbean.

Bi Russell, 47, aliona kile alidhani ni tundu kwenye sidiria yake na akakung’uta nguo yake ya ndani na ndipo alipoona mjusi jike akitembea.

Mkaguzi wa RSPCA alitumwa kushughulika na mjusi huyo ambaye alionekana kutokujeruhiwa baada ya kukaa kwenye nguo ya ndani.

Sandra Dransfield, wa RSPCA, alisema kumtoa mjusi huyo nchini Uingereza itakuwa kinyume cha sheria kwani ilikuwa spishi ambayo “haitaishi katika hali ya hewa yetu”. Mjusi amechukuliwa mtaalamu wa wanyama watambaao ambapo anasemekana anaendelea vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents