Michezo

Mkataba wa Aziz Ki Yanga sasa Freshi

Yanga imeshinda vita nyingine kubwa ya nje ya uwanja kimyakimya baada ya kumuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo wake mshambuliaji, Stephanie Aziz Ki lakini Arena tumeambiwa amesaini kwa kuwa masharti moja kwa viongozi.
Aziz ki
Aziz Ki amewaambia viongozi kwamba liwake inyeshe wamhakikishie kama watasaini straika wa maana kwenye dirisha lijalo na walipomthibitishia ndio akasaini mkataba ambao ni suala la muda tu atatangazwa kumaliza tetesi za yeye kutakiwa na Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates za Afrika Kusini na Esperance De Tunis. 
Taarifa kutoka ndani ya Yanga ambazo nimejiridhisha ni kwamba Aziz Ki ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo na amewaambia lengo lake ni kuhakikisha msimu ujao timu inapiga hatua zaidi kutoka hapo ilipo kwani kwasasa wanatumia nguvu kubwa zaidi kushinda mechi kubwa haswa za kimataifa.
Arena tunajua viongozi wamemhakikishia Aziz kwamba watashusha mastaa akiwewo mshambuliaji Prince Dube ambaye yuko Salasala jijini Dar es Salaam akiishi kwenye jumba moja la kifahari wakati akiendelea kushikilia msimamo wa kutaka kuachana na klabu yake ya Azam akidai hana furaha ya kuendelea kuwatumikia matajiri hao na tayari ameshakwenda TFF kuukana mkataba wake.
Credit: Wasafi Fm
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents