Habari

Mke wa mlanguzi wa dawa za kulevya ‘El Chapo’ ahukumiwa, aliwahi kumtorosha mumewe jela 

Mke wa mlanguzi sugu wa dawa za kulevya “El Chapo” Guzmán amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kufuatia kusaidia genge la uhallifu la Sinaloa.

Emma Coronel Aispuro walks out of Brooklyn Federal Court on July 17, 2019 after her husband's sentencing

Emma Coronel Aispuro, 32, alikubali makosa mwezi Juni kwa mashtaka yanayohusu njama ya usambazaji haramu wa dawa za kulevya.

Pia alikiri kumsaidia Guzmán kutoroka gereza la Mexico. Huenda angelikabiliwa na kifungo cha maisha gerezani, lakini waendesha mashtaka wa Marekani waliomba ahukumiwe kifungo kifupi baada ya kuonesha kuwa kujutia makosa yake.

Mume wake, 64, kwa sasa anahudumu kifungo cha maisha mjini Colorado.

Kulingana na nyaraka za mahakama, Coronel Aispuro, malkia huyo wa zamani wa urembo alikula njama na wanachama wengine wa genge la wahalifu la Sinaloa kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine, heroin, methamphetamine, na bangi nchini Mareakni, nakutakatisha fedha zilizotokana na uuzaji wa dawa hizo.

Mamlaka pia zinaamini kwamba Coronel Aispuro alifanya “jukumu muhimu ” katika mpango wa kumsaidia Guzmán kutoroka gereza lenye ulinzi mkali mwaka 2015 kwa kununua mali karibu na eneo hilo.

Guzmán aliweza kutoroka kupitia shimo lililochimbwa kupitia chini ya ardhi- iliyokuwa na mwangaza, vifaa vya kupumlulia na piki piki. Pia ilimpatia saa iliyowezeshwa kwa GPS- na kutuma ujumbe kwa washirika wake akiwa ndani ya jela.

Kwa miezi kadhaa hakujulikana ametorokea wapi hadi alipojitokeza kwenye mahojiano na mwigizaji Sean Penn.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents