Habari

Mkurugenzi TCAA akagua jengo jipya la kuongozea ndege Songea

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi amekagua jengo jipya la kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma.

Msangi amefanya ukaguzi huo jana Septemba 22, 2024 ambapo pamoja na ukaguzi huo pia amekagua miradi mingine katika kiwanja hicho ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 23, 2024.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo, wakati alipokuwa anawasili Uwanja wa Ndege wa Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024, kwa ajili ya kukagua jengo jipya la kuongozea ndege katika uwanja huo, ambalo linatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba 23, 2024 Mkoani humo. Picha na TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce, alipokuwa akiwatambulisha Maafisa wa TCAA kabla ya kutoa taarifa fupi ya jengo jipya la kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Jengo hilo pamoja na miradi mengine uwanjani hapo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024. Picha na TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce, alipokuwa akitoa taarifa fupi ya jengo jipya la kuongozea ndege, katika uwanja wa ndege Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Jengo hilo pamoja na miradi mengine katika kiwanja hicho inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024. Picha na TCAA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents