
Klabu ya Mlandege imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kumfunga Simba SC goli 1-0.
Mlandege inatetea Kombe hili la Mapinduzi mara ya pili mfululizo.
Wanaingia kwenye historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka Visiwani Zanzibar kuingia Fainali ya Mapinduzi mara mbili mfululizo na kuchukua kombe.
Huu ndio ushindi wao wa kwanza tangu kuanza kushiriki Mapinduzi msimu huu kwani mechi zilizopita wamesonga mbele kwa penati.
Simba imeingia Fainali hii ikiwa ni mara yao ya 10 wakati mara nne wamelitwaa taji huku Azam FC wakiwa wamelichukua mara tano.


