Habari

Mlango ulifunguliwa na mhudumu- Prof. Mbarawa

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ametoa ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022 Bukoba mkoani Kagere na kusababisha vifo vya watu 19.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa mlango wa ndege hiyo ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria.

Profesa Mbarawa amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa wananchi wanafanya shughuli za uvuvi jirani na eneo hilo la ajali walifika dakika 5 baada ya ndege kuanguka.

Amesema wananchi hao waliendelea na juhudi za kufungua mlango kwa nje, hali iliyompa ujasiri mhudumu wa ndege hiyo ya Precision Air na abiria kufungua mlango baada ya kuona nje kuna msaada ambao unaweza kuwasaidia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents