Mmzy alivyoijaza madini Ascent EP

Nyota anayekuja kwa kasi chini ya Lebo ya Kerae Records akachukwu Emmanuel Uche Maarufu kwa jina la Mmzy ni msaniii ambaye anakuja vizuri kupitia muziki aina ya Afrobeat akiwakilisha nchini Naijeria. Licha ya msanii huyo kuwa na ubora katika uandishi wake sauti yake ni moja ya kitu kinachomtofautisha na wasanii wengine ambao wamewahi kutokea katika muziki huko nchini Naijeria.

Mmzy ameachia rasmi Ep yake ya kwanza Iliyopewa jina la Ascent Ep yenye nyimbo 8 huku ikiwa na kolabo mbili akiwa ameshirikiana na msanii wa muziki Teni pamoja na Teri.

Ascent Ep imetayarishwa na watayarishaji watano ambaye ni Masterkraft,Echo The Guru,Cranker Mallo,Blaise Beats,Ozedikuz na nyimbo zote kukamilishwa na mtayarishaji Mix Monster.

Nyimbo Zote zimeandikwa na msanii Mmzy isipokuwa aliyoshirikiana na Teni pamoja na Terri na Bila kusahau wimbo namba 3,4,5,8.
Dominate ni moja ya wimbo wake unaofanya vizuri kwa sasa ukiwa unapatikana pia ndani ya Ep yake hiyo Iliyopewa jina la Ascent.

Unaweza kuwa wa kwanza kusikiliza kazi zote kutoka kwenye ep kupitia vyanzo mabli mbali ikiwemo,Apple music,BoomPlay,Spotify,audiomack na youtube.
Vilevile kwa taarifa Zaidi kuhusu mmzy unaweza kumfuata kupitia ukurasa wake wa Instagram @therealmmzy

Written by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button