Bongo5 ExclusivesHabariSiasa

Mnyika: Leo haki imeshinda udhalimu, dhulma na usaliti

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kesi ya msingi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 akiwemo Halima Mdee, waliovuliwa uanachama na chama cha CHADEMA hivyo kuruhusu taratibu zingine kuendelea.

Akizungumza na vyombo vya habari mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakili wa CHADEMA Peter Kibatala, amefafanua kuwa Mahakama pia imetupilia mbali maombi ya msingi ya kutaka kupewa kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama.

Aidha Kibatala ameeleza kuwa miongoni mwa sababu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kukosewa kwa jina la mjibu maombi namba moja ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA iliyosajiliwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameomba sasa sheria kufuata mkondo wake, akibainisha kwa sasa hawaoni sababu ya wabunge hao kuendelea kusalia bungeni. “Leo haki imeshinda udhalimu, dhulma na usaliti”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents