Michezo

Mo avunja Makundi Simba

Nje ya uwanja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed ‘Mo’ Dewji’ ameendelea na kazi ya kuunganisha timu kupitia vikao viwili vikubwa vilivyolenga kuvunja makundi na kuijenga upya Simba kama alivyoahidi wakati anarejea kuiongoza klabu hiyo.

Bilionea huyo alifanya kwanza kikao cha bodi mpya tangu alipoiunda kwa kuifumua ile ya zamani, kisha kila kitu kilienda sawa. Baada ya kikao hicho, MO alikutana na Baraza la Ushauri lenye watu wazito wakiwemo viongozi wa juu wa zamani kama Azim Dewji, Evans Aveva, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Kassim Dewji ‘KD’, Hassan Dalali, Swedy Mkwabi na aliyekuwa mgombea nafasi ya mwenyekiti Moses Kaluwa.

Kambi ya Simba Misri itakuwa ya wiki zisizopungua tatu kabla ya kurudi mapema Agosti kuwahi Simba Day ambapo mziki mzima utatambulishwa, kisha itajiandaa na mechi za Ngao ya Jamii zitakazopigwa kati ya Agosti 8-11 na siku chache kuanza vita ya Ligi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents