Michezo

Monalisa atangazwa kuwa Msemaji Simba Queens

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara Simba Queens, wamemtangaza rasmiĀ Msanii wa filamu Bongo, Monalisa kuwa Msemaji wa timu hiyo.

Kupitia kwa Mlezi wa Simba Queens, Fatema Dewji amemtambulisha mwanadada huyo nguli katika tasnia ya Filamu nchini na mwenye mafanikio makubwa kwenye upande huo kuwa Msemaji wa timu hiyo.

”Mlezi wetu Fatema Dewji (@fatemagdewji) amemkaribisha rasmi Monalisa (@monalisatz) kama msemaji wa simba queens tunaimani Monalisa atafanya kazi nzuri katika kueneza taarifa zote zinazohusiana na Simba Queens kwenye jamii yetu. Kwa uzoefu wa Monalisa tunaimani atakwenda kuwa msemaji bora wa timu yetu na uzoefu wake aliokua nao katika jamii. Karibu Simba Queens Msemaji Wetu šŸ‘øšŸ¦ @monalisatzĀ  ,” Taarifa kutoka katika timu hiyo ya Simba Queens.

Simba Queens Ijumaa hii ya Machi 5, 2021 itashuka uwanjani kuwavaa watani wao wa jadi Yanga Princess kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake katika dimba la Uhuru.

Kwenye msimamo wa Ligi hiyo maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier LeagueĀ  Yanga inaongoza kwa kuwa na jumla ya alama 38, nafasi ya pili ikichukuliwa na Simba Queens wenye pointi 36 huku matokeo ya mchezo wa Ijumaa hii watakapokutana yataamua Wanajangwani kuendelea kuongoza Ligi ama Msimbazi kuchukua msukani wa msimamo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents