Habari

Mongella awataka Arusha kutumia fursa kwenye afya

Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongella amewataka wananchi wa Jiji hilo kutumia wiki ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya upimaji afya pamoja na ushauri wa kitaalamu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo, Mh. Mongella amesema kwamba maadhimisho hayo yanayofanyika nchi nzima, Kitaifa yanatarajiwa kuadhimishwa Arusha  katika uwanja wa Sheikh Amri Abeiid, huku Waziri wa Afya Doroth Gwajima akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Aidha ameeleza kwamba maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Innocent Bashungwa.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy Mwalimu pamoja na Waziri Joyce Ndalichako wametajwa kuhudhuria maadhimisho hayo yatakayoanza Novemba 6 hadi 13.

Pamoja na hayo, Mh. Mongella amesema shughuli zitakazofanyika ni upimaji wa afya, mazoezi, ushauri wa kuwa na mtindo mzuri wa maisha ikiwa ni pamoja na elimu ya vyakula nk.

Mbali na hayo, kiongozi huyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia swala la afya hasa magonjwa yasiyo ambukiza kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya afya nchi nzima.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents