
Kocha Msaidizi wa KenGOld, Omary Kapilima amezungumzia hali ya kikosi chake akisema:
“Wachezaji wote wapo sawa sawa kasoro Bernard Morrison ambaye ana changamoto, anamalizia matibabu ili aanze mazoezi, lakini waliobaki wote wapo vizuri.
.
“Katika mechi 16 tumepata alama sita, baada ya ligi kusimama, hivyo ni kama tunaaza upya kesho (leo) tukitegemea kupata alama tatu.”