Siasa

Morocco ilijaribu kudukua simu ya rais wa Ufaransa Macron

Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema kuwa huduma za usalama za Morocco zilifanya udukuzi wa simu ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kutumia waya wa udukuzi uliotengenezwa nchini Israeli -Pegasus spyware.

Makundi ya kutetea haki za binadamu Forbidden Stories na Amnesty International yanasema kuwa Rabat ilitambua simu ambayo Rais Macron amekuwa akiitumia tangu mwaka 2017.

Haijafahamika wazi iwapo waya huo wa Pegasus uliwahi kutumiwa.

Mawaziri kadhaa pia walidaiwa kufuatiliwa, akiwemo waziri mkuu wa zamani Edouard Philippe.

Namba zao za simu zilikuwa miongoni mwa namba 50,000 ambazo zilikuwa zimezoorodheshwa kati ya namba zinazoweza kudukuliwa .

Ripoti hiyo ilisema kuwa ufuatiliaji wa kidigitali wa nyaya za udukuzi wa Pegasus ulikuwepo kwenye makumi ya nambari hizo za simu.

Watengenezaji wa Pegasus, NSO Group, wanasema huuza kifaa hicho kwa serikali zilizochunguzwa kwa ajili kukabiliana na uhalifu na ugaidi.

Related Articles

Back to top button