Michezo

Mourinho amkingia kifua Rashford baada ya kuoneshwa kadi nyekundu dhidi ya Burnley

Mourinho amkingia kifua Rashford baada ya kuoneshwa kadi nyekundu dhidi ya Burnley

Kocha wa Manchester United na raia wa Ureno Jose Mourinho ameamua kumkingia kifua winga wa klabu hiyo Marcos Rashford baada ya kuoneshwa kadi nyekundu jana katika mchezo dhidi ya Burley na kusababisha kuikosa michezo mitatu ya klabu hiyo.

Winga huyo aliigarimu timu yake kucheza pungufu kwa takribani dakika 19 baada ya kuoneshwa kadi hiyo mnamo dakika ya 71 kwa kumpiga kichwa beki wa Burley phil Bardsley.

Katika mchezo huo Manchester United walifanikiwa kushinda kwa jumla ya goli 2-0 kwa magoli yaliyofungwa na mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ua Ubelgiji Romelu Lukaku dakika ya mnamo dakika ya 27 na 44.

Baada ya mchezo huo kumalizika katika mahojiano aliyofanya na sky Mourinho alionekana kumkingia kifua mchezaji wake kwa kusema kuwa :-

“Sijui ni nini kilichotokea ila.. Ningeweza kusema kuwa ni uliotokea ni ujinga.kwa maana nyingine Ilikuwa mtoto na mtu mwenye uzoefu sana kwa muda mrefu kwenye ligi. Bardsley amekuwa katika mchezo soka kwa miaka 20 na Marcus ni kijana mwenye ujinga bado ana utoto mwingi anakua”

Baada ya ushindi wa jana United sasa imeshika nafasi ya 10 kwa kuwa na alama 6 katika michezo 4 ilicheza ikishinda 2 na kupoteza 2.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents