Mpaka sasa tunaweza kusema Man City 1 – 0 UEFA, pigo kwa timu zinazotafuta ‘Top Four’ kwa tochi

Klabu ya Manchester City imefutiwa adhabu ya kufungiwa kushiriki mashindano ya UEFA Champions League/Europa League kwa miaka miwili, baada ya kushinda rufaa katika mahakama ya michezo inayojulikana kama Court of Arbitration for Sport (Cas).

Matokeo hayo ni kama Manchester City imeshinda vita vyake dhidi ya UEFA na kuonyesha kuwa hawakuwa na hatia bali kuhumu iliyotolewa mwezi Februari dhidi yao ilikuwa ni uonevu.

Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo Pep Guardiola ameonekana akishangilia akiwa sanjari na benchi lake la ufundi mapema asubuhi ya leo.

Miamba hiyo ya soka kutoka Premier League imefanikiwa kushinda rufaa hiyo baada ya kufungiwa kutokana na kuvunja kanuni za sheria ya fedha (Financial Fair Play). ‬

Kushinda kwa zuio hilo kumezusha taharuki kwa mashabiki wa baadhi ya klabu za Premier League kama Manchester United, Chelsea, Leicester ambao walikuwa wanawania nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ili kupata fursa ya kushiriki Champions League jambo ambalo linaonekana kuwa limegonga mwamba.

Kauli ya baadhi ya mashabiki ambao wameandika baada ya City kupata ushindi wa rufaa yao.

Related Articles

Back to top button